MAAMUZI MAGUMU YANAWEZA KUBADILI HALI TATA
by Bishop Josephat Njige
Katika kitabu cha Mathayo 14:25-31, Muda mfupi baada ya Yesu kuwalisha watu 5,000 kwa mikate mitano na samaki wawili, aliamua kuchukua uamuzi mgumu ili kuwafundisha wanafunzi wake juu ya uungu wake maana walionekana kutoshitushwa na muujiza wa mikate. Wakiwa wamelazimishwa kuvuka Bahari ya Galilaya bila Yesu wanakutana na upepo wa mbisho uliotishia maisha yao. Ghafla Yesu anawatokea akiwa anatembea juu ya maji na kuwafanya wapate hofu zaidi. Baada ya kujitambulisha kwao, Petro anamsihi amuruhusu atembee juu ya maji kuelekea alipo Yesu Kristo ili kuthibitisha kama kweli ndiye Yesu mwenyewe, tukio hili lilibadili kabisa mtazamo na imani ya mitume wote juu ya Yesu na hatimaye wakamwabudu na kukiri kuwa Yeye ndiye mwana wa Mungu. Maamuzi magumu ya Petro yanamuweka karibu zaidi na Yesu na kumfanya aheshimiwe na wenzake. Fanya maamuzi magumu leo ili hali yako ya leo na kesho yako ibadilike. Fuatilia somo hili kwa umakini utabadili hatima yako.